Monday, December 18, 2017

Kitabu kinachoelezea maisha ya wasichana waliotekwa na Boko haram tangia 2014 chatoka rasmi.

Kitabu kinachoelezea kuhusiana na maisha ya wasichana wadogo wanaotoka Chibok nchini Nigeria ambao walitekwa nyara na kundi la Boko haramu tangia mwaka 2014 wakati walipokuwa wakitoka shuleni kimetoka rasmi kikielezea historia nzima ya wasichana hao na kila walichokutana nacho wakiwa mateka.

Kitabu hicho kilichopewa jina la Stolen girls kimeshaanza kupata umaarufu mkubwa baada ya kuanza kupostiwa na wanafilosophia wakubwa duniani baada ya kutoka kwake akiwema Malala Yousafzai binti wa Pakstan aliyepigwa risasi kwa kutetea haki za watoto wa kike kusoma nchini humo.



Share:

Sunday, December 10, 2017

Mange Kimambi atumia akaunti nyingine ya Instagram kuendeleza mashuti mitandaoni.

Mwanamke maarufu kwa kuwakosoa wanasiasa wa Tanzania Mange Kimambi ambaye alikuwa amefungiwa account yake sasa amekuja na account mpya ya Instagram. Mange aliruka live ili kuwadhihirishia watu kuwa ni yeye katika account na amekwisha anza kuitumia account hiyo kwa shughuli zake za kawaida.

Share:

Tuesday, December 5, 2017

Keisha achaguliwa kuwa mgombea ujumbe halimashauri kuu Chama cha mapinduzi NEC.

Msanii wa muziki Keisha amepata fursa ya kuchaguliwa kuwa mgombea ujumbe katika tume ya taifa ya chama cha mapinduzi NEC.

Share:

Watu 5 waliiongoza kuwa na retweet nyingi mwaka 2017.

Katika mtandao wa twitter watu huweza kushare vitu vya wenzao kwa kuretweet ujumbe uliopostiwa. Hii ni orodha ya walioongoza kwa kupata retweet nyingi mwaka 2017.
1. Mchezaji wa mpira wa miguu wa kimarekani Carter Wilkerson. Carter pia ni miongoni mwa wapenzi wa kipindi cha Television kiitwacho Wendy's show ambapo carter alipost akiomba kupewa kuku na alipewa mashrti ya kufikisha retweet millioni 18 japokuwa hakuzifikisha lakini aliweza kufikia retweet zaidi ya millioni 3.6 jambo linalomfanya kuongoza orodha hiyo mwaka 2017.

2. Ariana Grande baada ya kupost ujumbe wa kusikitishwa katika shambulio la bomu kwenye show yake aliyokuwa akiifanya Manchester uingereza.
3. Mchezaji wa mpira Jermain Defoe akiomboleza baada ya kifo cha shabiki maarufu mtoto wa mpira aliyefariki.
4. Ujumbe wa Barack Obama kuhusu haki na usawa kwa watu wote.

5. Mchezaji wa zamani wa mpira Andy Johson's kusapoti kampeni ya kiafya .



Share:

Sunday, December 3, 2017

Mashindano ya kuibua vipaji ya Dance Kitaa yaanza rasmi jijini Mwanza.

Mashindano ya Dance Kitaa jijini Mwanza yameanza rasmi jana katika viwanja vya busket ball vya Mirongo ambapo makundi ya vijana wenye vipaji vya kudance yaliweza kujisajili na kushiriki katika mashindano hayo..... Kupitia TrendTz News blog tutaendelea kukuletea mashindano hayo katika kila hatua.

Share:

Chrisbrown aanika mahusiano yake mapya hadharani na staa wa Pop Indonesia katika birthday ya Dj Khaled.

Mwanamuziki Chrisbrown siku ya jana ameamua kuudhihilishia umma kuhusiana na mahusiano yake mapya pamoja na mwanamuziki maarufu wa Pop nchini ndonesia Agnez Mo (31) baada ya mastaa hao kuonekana ndani ya mahaba mazito katika birthday ya Dj Khaled.



Chrisbrown aliachana mwanamitindo Karuetche ambaye walidumu katika mahusiano kwa muda na baadae karuetche alianza kumtuhumu Chrisbrown kwa kumtishia mara kadhaa wakati walipokuwa katika mahusiano.  Baada ya kutengana na Karuetche ndipo Chrisbrown alipoanza kupost picha akiwa na Agnez mara kadhaa mitandaoni huku ikionekana kama ni kutangaza jina la brand yake ya nguo inayoitwa Black Pyramid hadi jana alipoanika mahusiano hayo hadharani.


Share:

Breaking News

Contact Us

Name

Email *

Message *

Translate

Total Pageviews