Tuesday, May 23, 2017

UTAFITI: Vitamini D husaidia na kuimalisha kinga kuzuia saratani ya matiti.

Vitamin D ina faida nyingi muhimu za kiafya mwilini na utafiti wa hivi karibuni umebaini kuwa vitamin hiyo ndiyo msingi mkubwa wa kuzuia magonjwa mbalimbali mwilini kwa sababu kiasia cha asilimia 10 ya vinasaba (genes) vya mwili wa binadamu vinaitegemea vitamin hii kufanya kazi yake, kikiwemo kinasaba kinachohusika na uzuiaji na udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza na yale ya uvimbe.


Katika utafiti huo ambao pia umeelezewa kwa kina na Dr Mercola wa nchini Marekani katika mtandao wake imeoneshwa kwamba ukiwa na Vitamin D ya kutosha mwilini, Kolestrol mbaya hushuka na pia huongeza mara mbili uwezo wa mwili kujikinga na saratani ya matiti.
Vilevile utafiti huo umebainisha na kugundua kwamba, kuna uhusiano mkubwa kati ya upungufu wa Vitamin D mwilini na watoto wanaozaliwa na matatizo ya ubongo. Ugunduzi huu ni muhimu sana, hasa kwa akina mama waja wazito, kwani madhara ya kuwa na upungufu mkubwa wa Vitamin D unaweza kusababisha kuzaa mtoto mwenye mtindio wa ubongo.

Katika makala yake, Dk. Mercola ameeleza kuwa tangu miaka ya 2000, utafiti kuhusu umuhimu wa Vitamin D umeongezeka sana. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2012, tayari zilikuwa zimeshachapishwa tafiti karibu 34,000 na kuna kumbukumbu (references) za kitabibu zaidi ya 800 ambazo zinaonesha uwezo wa Vitamin D katika kuzia saratani.


Kwa mujibu wa mwanzilishi wa mtandao ujulikanao kama GrassrootsHealth, Bw. Carole Baggerly, kiasi cha asilimia 90 ya saratani ya kawaida ya matiti ina uhusiano mkubwa na upungufu wa Vitamin D mwilini.
Katika jarida la ‘Anticancer Research1’, toleo la Machi mwaka huu, kumechapishwa utafiti wa wagonjwa wa kansa ya matiti waliopimwa kiwango cha Vitamin D. Iligundulika kwamba wenye kiasi kingi cha Vitamin D wana uwezekano wa kupona na kuishi kwa muda mrefu mara mbili ya wale wenye kiwango cha chini cha Vitamin hiyo. 

Vitamin D hupatikana kwa kuota jua, hasa lile la kati ya saa moja asubuhi hadi saa sita mchana, hata kwa muda wa angalau dakika kumi tu pia ulaji wa mboga za majani hongeza kwa wingi vitamini hiyo kwa njia ya kiasili zaidi.


Share:

0 comments:

Post a Comment

Breaking News

Contact Us

Name

Email *

Message *

Translate

Total Pageviews