Thursday, November 30, 2017

Historia ya siku ya UKIMWI duniani.

Siku ya UKIMWI duniani huadhimishwa kila tarehe 1 December na ilichaguliwa kuwa siku ya UKIMWI kutokana na tarehe hiyo kuwa ndiyo siku ambayo kirusi cha UKIMWI kilitambulika rasmi mwaka 1981. Takwimu zinaonyesha kuwa toka mwaka 1981 hadi 2007 watu zaidi ya milioni 25 walikuwa tayari wamekwishafariki kutokana na Ukimwi. Mwaka 2007 peke yake walifariki milioni 2, kati yao watoto 270,000.

Siku hiyo ilichaguliwa rasmi mwaka 1988 wakati wa Mkutano wa dunia wa mawaziri wa afy kuhusu mpango wa kuzuia UKIMWI. Kuanzia hapo siku hiyo imekuwa ikikumbukwa rasmi na serikali pamoja na mashirika mbalimbali.
Alama inayotambulisha ugonjwa huo.


Toka mwaka 1988 hadi 2004, Siku ya Ukimwi Duniani ilikuwa ikiratibiwa na Shirika la Umoja wa mataifa la mwaswala ya UKIMWI (UNAIDS). Mwaka 2005 UNAIDS iliipa Kampeni ya kupambana na UKIMWI (the World AIDS Campaign) wajibu wa kuratibu siku hiyo na kila mwaka siku hiyo huadhimishwa sambamba na ujumbe maalumu unaolenga kupambana na ugonjwa huo.

Kwa hapa Tanzania siku hii inaadhimishwa leo kitaifa katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar ew Salaam huku mgeni rasmi akiwa makamu wa raisi Mama Samia Suluhu Hassan huku kauli mbiu inayotumiwa kimataifa ikiwa ni "Everybody counts" ikihimiza haki za kiafya kwa wagonjwa pamoja na uwajibikaji wa kila mmoja katika jamii kupambana na ugonjwa huo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Breaking News

Contact Us

Name

Email *

Message *

Translate

Total Pageviews