Wednesday, April 26, 2017

Fahamu hasara za ulaji wa nyama, ikiwemo kupata ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu na kansa ya utumbo.

Utafiti unaonyesha ulaji wa nyama kiujumla una madhara katika mwili wa binadamu japokuwa ulaji wa nyama nyekundu kama nyama ya ng'ombe, mbuzi au nguruwe una madhara makubwa sana kuliko ulaji wa nyama nyeupe hizi ni baadi ya hasara za kula nyama .


Hatari ya kupata ugonjwa wa alzheirs disease,  huu ni ugonjwa wa akili ambao huwapata watu wengi uzeeni na dalili yake ikiwa ni kupoteza kumbukumbu kabisa. Wanasayansi wanaamini protini inayopatikana kwenye nyama kwa jina la Tau and beta-amyloid huharibu mishipa ya fahamu ya kwenye ubongo na kuchangia  ugonjwa huu hivyo ulaji wa nyama nyingi husogeza karibu zaidi uwezekano wa kupata ugonjwa huu.
 Kansa ya utumbo mkubwa, nyama nyekundu kwa mfano nyama ya mbuzi, ng'ombe na nguruwe ikiliwa inakaa masaa mengi zaidi kwenye mfumo wa chakula wa binadamu tofauti na vyakula vingine. Utafiti unaonyesha limbikizo hilo linaambatana sana na hatari ya kupata ugonjwa wa kansa ya utumbo mkubwa. Lakini madhara  haya yameonekana kutokuwepo kwa kula nyama nyeupe kama nyama ya samaki, kuku au baadhi ya ndege.
 Hatari ya kupata magonjwa ya moyo, nyama ina kitu kinaitwa lehemu kitaalamu kama cholesterol, hii hukaa kwenye mishipa ya damu ya binadamu na kusababisha damu kushindwa kupita vizuri..hii husababisha viuongo muhimu vya mwili kama moyo kukosa damu ya kutosha na kuanza kushindwa kazi. Japokua cholesterol ni muhimu kwenye mwili wa binadamu lakini inayotengenezwa na mwili inatosha hii inayoongezeka kutoka kwenye nyama ni hatari sana pia nyama nyekundu ina cholesterol nyingi zaidi.
Ugonjwa wa kifafa, minyoo inyopatikana kwenye nyama ya nguruwe kitaalamu kama taenia solium hupanda mpaka kwenye ubongo na kuharibu mishipa ya fahamu ya ubongo hali ambayo husababisha kifafa kwa watu ambao hawakuzaliwa nacho kabisa. Halii hii inaweza kuzuiliwa kwa kupika nyama hiyo kwa muda mrefu sana mpaka iive ndiyo iweze kuliwa.
 Unene uliopitiliza,  Nyama nyekundu ina kiwango kikubwa cha mafuta ambacho watu wengi hula mafuta hayo kama yalivyo mfano kwenye nyama ya nguruwe. Unene  na kitambi ni hatari sana kwani husababisha matatizo mengi ya kiafya na kisaikolojia, vifo vya ghafla vikiwa hatari zaidi kwenye swala la unene, Hivyo mlaji wa nyama anatakiwa kufanya mazoezi zaidi ili kupunguza mafuta hayo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Breaking News

Contact Us

Name

Email *

Message *

Translate

Total Pageviews