Wednesday, August 9, 2017

Mfahamu Malala Yousafzai binti aliyepigwa risasi utotoni kwa kutetea haki ya wasichana kupata elimu Pakistan.

Malala Yousafzai alizaliwa tarehe 12 mwezi wa 7 mwaka 1997 katika mji mdogo wa Swat ulioko kusini magharibi mwa nchi ya Pakistani. Baba yake anaitwa Ziauddin Yousafzai alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakipigania watoto kupata elimu.

Malala alianza kujishughulisha na harakati za kutetea elimu mwaka 2009,mwaka ambao jeshi la Talibani lilikuwa limeshikilia wilaya aliyokuwa akiishi ambapo Malala alianza kuandika blog kwa ajili ya kueleza kuhusiana na uwoga anaoupata shuleni kuwa shule yake inaweza ikavamiwa wakati wowote ule,malala na babayake waliwahi kupokea vitisho vya kuuwawa mara kadhaa lakini hawakuogopa na kuendelea kutetea haki ya kupata elimu.
Mwaka 2011 Malala alipewa tuzo ya amani ya vijana ya nchini Pakistani (National Youth Peace Prize) na baada ya hapo akatangazwa na Askofu Desmond Tutu kugombea tuzo ya amani ya watoto ya kimataifa ya watoto ( International Chirdren's Peace Prize).
Tarehe 9 mwezi wa 10 mwaka 2012 siku ambayo Malala na rafiki zake walipokuwa wakitoka shuleni watu waliofunika nyuso zao walivamia gari yao ya shule na kumpiga Malala risasi kichwani, Baadaye Malala alipelekwa hospitalini na baada ya muda alihamishiwa katika jiji la Birmingham nchini Uingereza kwa ajili ya matibabu zaidi na mwezi wa kwanza mwaka 2013 Malala aliruhusiwa kutoka hospitalini na kuungana na familia yake iliyohamia tayari nchini Uingereza.
 Mwaka huo huo Malala na baba yake walianzisha mfuko unaoitwa Malala Fund unaowasaidia wasichana kupata elimu. Tarehe 10 mwezi wa 12 Malala alipata tuzo ya kimataifa ya amani ya NOBEL na alichangia zaidi ya dola za kimarekani $500,000 katika kuanzishwa kwa shule za wasichana nchini Pakistani. Mpaka sasa mfuko wa Malala Fund unaendelea kupigania haki za elimu kwa wasichana.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Breaking News

Contact Us

Name

Email *

Message *

Translate

Total Pageviews