Sunday, October 1, 2017

Fahamu madhara ya kuchora Tatoo mwilini.

Tatoo hutokana na uwekaji wa wino ndani ya ngozi kitaalamu hufahamika kama Dermis na kubadilisha rangi ya ngozi kabsa.
Tatoo hupendwa na watu wengi hasa hasa vijana katika nchi zinazoendelea ikiwemo nchi ya Marekani inayosemekana kuongoza kwa  kuwa na idadi kubwa ya watu waliochora Tatoo duniani. Lakini kuna madhara mengi unayoweza kuyapata kutokana na uwekaji wa wino huu ndani ya ngozi.


Allergy ya ngozi.
Baadhi ya wino unaotumika katika uchoraji wa tatoo hasa wino wa rangi ya njano na nyekundu huwa na chembechembe za madini ya Cadinium Silfide ambayo husababisha allergy katika ngozihasa pale ambapo chembe hizo zinapokutana na mwanga wa jua hivyo kusababisha ngozi kuvimba na kubadilika hususa ni sehemu zinazozunguka tatoo hiyo.


Maambukizi ya magonjwa.
Wakati wa uchoraji wa tatoo kuna uwezekano wa kupata tetenus lakini pia maambukizi ya magonjwa mbalimbali yanayoweza kuenea kwa njia ya damu ikiwemo Hepatits ama homa ya ini.

Kuziuwa kuchangia damu.
Mtu mwenye tatoo huzuiwa kuchangia damu mpaka pale itakapopita miezi 6 ama 12 baada ya kuchora tatoo ili kuweza kukwepa baadhi ya maambukizi yanayoweza kuambukizwa kwa njia ya damu kwenda kwa muongezewaji. Kuna baadhi ya virus ambavyo mtu anaweza kuvipata wakati wa kuweka tatoo na endapo damu ya mtu huyo ikiwekwa kwa mwingine naye pi hupata virusi hivyo, mfano ni Hepatits B virus.

Kukosa fursa mbalimbali.
Zaidi ya kupata madhara ya kiafya pia unaweza kupata madhara ya kijamii ikiwemo kukosa fursa mbalimbali za kazi kwa sababu baadhi ya makampuni hayawaajili watu ambao wana michoro ya tatoo mwilini. Pia huwezi kupata kazi katika vyombo vya usalama mfano jeshi, polisi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.


Share:

0 comments:

Post a Comment

Breaking News

Contact Us

Name

Email *

Message *

Translate

Total Pageviews