Thursday, March 2, 2017

RIPOTI: Polisi nchini Uphilipino watuhumiwa kupandikiza ushahidi feki pamoja na mauaji ya watu zaidi ya 7,000 katika vita dhidi ya madawa ya kulevya.

Vita dhidi ya madawa  ya kuleva nchini Uphilipino imeendelea kwa kasi hasa baada ya Raisi wa nchi hiyo Rodrigo Duterte kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha na kupambana na madawa hayo. Hapo awali jeshi la polisi la nchi hiyo lilitoa taarifa inayoonyesha vifo 25,000 vilivyotokea wakati wa oparesheni mbalimbali zilizohusisha kurushiana risasi baina ya polisi na wahalifu. Lakini kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rigths Watch  ambayo ilisomwa na mwandishi wa ripoti hiyo Peter Bouckaert imewatuhumu Polisi nchini Uphilipino kwa kugushi ushahidi pamoja na mauaji ya watuhumiwa wa  madawa ya kulevya zaidi ya 7,000 kuanzia mwaka jana hadi sasa. 



Shirika hilo pia limesema kuwa limefanya uchunguzi katika matukio 24 yaliyosababisha vifo 32 katika mji mkuu wa nchi hiyo Manila na pia limeongea na ndugu wa karibu wa marehemu pamoja na mashahidi mbalimbali  ili kukamilisha ripoti yao.
 Mwezi ulioisha Raisi wa nchi hiyo alihamisha mamlaka ya kupambana na dawa hizo kutoka kwa Jeshi la Polisi nchini humo na kuwapa mamlaka inayohusika na kupambana na dawa hizo nchini humo lakini hivi karibuni raisi huyo amesema anampango wa kuwarudisha polisi tena katika vita hiyo.


Share:

0 comments:

Post a Comment

Breaking News

Contact Us

Name

Email *

Message *

Translate

Total Pageviews