Friday, July 28, 2017

Baraka da prince atoa sababu ya kutoka Rockstar4000 kuwa ni kutokuwa serious kwa management ya Alikiba.

Baada ya kuondoka katika management ya RockStar4000 leo Baraka Da Princeameongea sababu zilizo mfanya kuondoka kwake kupitia EATV (Enews).
“Nimeamua kufanya hivyo kwa sababu hii ndiyo kazi yangu na mwisho wa siku hii mimi ndiyo kila kitu na sina kazi nyingine, kwa hiyo nikiona kuna vitu havipo ‘serious’ na havipo ‘sure’ kwa upande wa watu ninaofanya nao kazi sina budi kujiengua na kufanya mwenyewe. Nipo sawa na hakuna mtu ambaye anaweza kuniingilia juu ya hilo mwisho wa siku mimi ndiyo ninajua kazi ninayofanya na ugumu wake katika kujenga ‘brand’ yangu, najua ugumu wa kila kitu ‘so’ haya ni maamuzi yangu....mimi ndiyo mwenye kauli ya mwisho. Sitaki kuongelea masuala ya mikataba kwa sababu kipindi nina saini tokea awali sikuweza izungumzia wakati naingia kwa hiyo sitasema lolote juu ya hilo kwa sasa”,alisema Baraka Da Prince.
Kwa upande mwingine, Baraka amesema yeye hafanyi muziki kwa ajili ya menejementi bali anafanya muziki kwa mashabiki wanamuwezesha kwa kumlipa katika nyimbo zake wanazozipakua katika mitandao.

 
Share:

0 comments:

Post a Comment

Breaking News

Contact Us

Name

Email *

Message *

Translate

Total Pageviews