Tangawizi ni mmea kati ya mimea mingi yenye maajabu, Mmea huu unaweza kutumika kama dawa na kutibu magonjwa mengi tu zaidi ya 72 yaliyo ndani ya miili yetu.
Utafiti wa kitaalam unaonyesha kuwa ndani ya zao la Tangawizi kuna vyanzo vikubwa vya madini ya magenisium, manganese, Selenium, Iron, Vitamini B6 ambavyo kwa pamoja huleta kinga tosha kwa baadhi ya maladhi ikiwemo maladhi ya ngozi japokuwa wataalam wamethibitisha Tangawizi kuwa na msaada mkubwa katika mwili wa binadamu kwa mmea huo kuwa na uwezo mkubwa katika kutibu magonjwa mengi sana yanayotusumbua.
Maumivu ya tumbo:Tangawizi inatumika kutuliza maumivu ya tumbo, yanayotokana na matatizo ya usagaji chakula, kuharisha, kuvimbiwa, n.k. Inapotumiwa katika chakula tangawizi husaidia usagaji chakula. Aidha tangawizi humuongezea mtu hamu ya kula.
Matatizo ya Moyo: Tangawizi hupunguza kiwango cha mafuta mwilini hivyo humsaidia na kumwepusha mtu na matatizo ya moyo kwa kuyeyusha mafuta katika mishipa ya kusukuma damu.
Matatizo ya Kupumua: Huondoa homa ya mafua, hutumika kutibu pumu, na pia kufungua mfumo wa upumuaji hasa inapotumika pamoja na asali.
Maumivu:uondoa maumivu ya misuli kwa sababu tangawizi ina uwezo mkubwa wa kulainisha misuli hasa pale inapopakwa sehemu iliyoathirika.
Maumivu ya Hedhi: Hupunguza maumivu ya wakati wa hedhi kwa wanawake.
Malaria: Husaidi kutibu Malaria na Homa ya Manjano.
Nguvu za Kiume: Tangawizi husaidia kuongeza nguvu za kiume kwa kutibu tatizo la mwanamume kutoa shahawa haraka.
Figo:Inaaminika kuwa tangawizi inatibu tatizo la vijiwe vya kwenye figo.
Saratani: Hutumiwa na wataalamu wa kimatibabu katika tiba ya saratani.
0 comments:
Post a Comment