Thursday, June 29, 2017

Ripoti ya polisi yamuonyesha nyota wa tenesi duniani Venus William chanzo cha ajali iliyopelekea kifo cha mtu Florida.

Polisi jijini Florida wametoa ripoti inayomuonuesha staa wa tenesi duniani Venus Williams kuwa ndiye chanzo cha ajali iliyopelekea kifo cha mtu mmoja anayefahamika kama Jerome Barson iliyotokea siku ya tarehe 2 mwezi wa 6 jijini hapo.

Ripoti hiyo imedai kuwa staa huyo wa tenesi aliyekuwa akiendesha gari lake aina ya Toyota Sequoia SUV hakufata sheria za barabarani na kuingia katika njia wakati taa nyekundu zikiwa zimewaka jambo ambalo lilimsababisha kuparamia gari iliyokuwa inaendeshwa na Jerome hatimaye kumsababishia majeraha makubwa yaliyopelekea kifo chake wiki mbili baadae.

Hata hivyo kamanda wa idara za polisi jijini hapo Paul Roders amesema kuwa licha ya kutolewa kwa ripoti hiyo bado tukio hilo lipo katika uchunguzi na uchunguzi utakapo kamilika Venus Williams atafunguliwa mashitaka hayo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Breaking News

Contact Us

Name

Email *

Message *

Translate

Total Pageviews