Friday, June 9, 2017

Kitimoto yapigwa marufuku Dodoma baada ya mlipuko wa homa ya nguruwe.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Bi.Christina Mndeme amepiga marufuku uingizwaji na uchinjwaji wa nguruwe kiholela pia amewataka wakazi wa Dodoma mjini kula nyama ya nguruwe iliyopimwa na wataalamu wa afya ili kuepuka mlipuko wa homa ya nguruwe.
Bi. Christina Mndeme alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza na madiwani na watendaji wa Manispaa ya Dodoma ambapo alisema hadi sasa zaidi ya nguruwe 200 tayari wameshakufa kutokana na mlipuko huo.
Ninawaagiza nyinyi madiwani pamoja na watendaji hakikisheni mnatoa elimu iliyo sahihi kwa uwazi bila kificho, ukizingatia kuwa ugonjwa huu unaua tena kwa asilimia mia moja, hivyo ni marufuku kuingiza ndani ya wilaya hii na wala kuchinja pasiporuhusiwa na wataalamu wa afya,” alisema Bi. Christina.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Breaking News

Contact Us

Name

Email *

Message *

Translate

Total Pageviews