Tafiti zinaonyesha kuwa ulaji wa Tango huleta faida nyingi mwilini na kuufanya mwili wa binadamu kuwa imara zaidi moja wapo ya faida za tango huondoa sumu mwilini(toxins) , maji yaliyopo kwenye matango husaidia kusafisha na kuondoa sumu ndani ya mwili, Pia ulaji wa matango mara kwa mara huyeyusha mawe kwenye figo na kusaidia figo kufanya kazi yake kwa ufasaha zaidi.
Tafiti zimeonyesha kuwa matango yanauwezo wa kumsaidia mtu kuepukana na kansa kutokana na kuwa na madini ambayo husaidia uboreshwaji wa kinga za mwili dhidi ya kansa mbali mbali ikiwemo kansa ya titi na tezi dume.
Matango yanaongeza afya ya joint zako na kuondoa maumivu ya kwenye magoti na arthritis Kwa kuwa na madini mengi aina ya silica ambayo husaidia kuondoa maumivu ya magoti kwa kushusha level ya uric acid Pia matango yana madini ya silica ambayo hufanya nywele na kucha kung'aa zaidi.
0 comments:
Post a Comment