Mchanga huu unaaminika kuwa ni matokeo ya mlipuko wa Volcano kwenye mlima Oldonyo Lengai uliorushwa maeneo ya karibu na mlima ulikuwa kwenye eneo la kreta ya Ngorongoro karibia miaka 3,000 iliyopita lakini baadaye mlima huo ulizama na kutengeneza bonde la Ngorongoro tunalolishuhudia hivi sasa. Inaaminika kuwa mchanga huo wenye nguvu za uvutano (Sumaku) ulianza safari zake katika muda usiojulikana kutokana na kutokuwepo kwa takwimu sahihi za safari hiyo kwa miaka ya nyuma.
Mchanga huo hutembea kwa kusukumwa kwa upepo huku ukiwa umejikusanya pamoja bila kuacha mabaki nyuma kiasi kwamba mgeni hawexi kutambua ni sehemu gani mchanga ulipokuwa awali mpaka msaada wa wenyeji katika eneo husika.
Wamasai wanaamini kuwa mchanga huo ni mtakatifu hivyo huenda sehemu uliyopo mchanga huo kwa ajili ya kufanya matambiko ili kuweza kufanikiwa yale wanayoyaomba katika imani yao.
0 comments:
Post a Comment