Tuesday, August 1, 2017

Waziri mkuu aagiza kukamatwa na kuhojiwa Meya mstaafu jiji la Mbeya kwa tuhuma za kulisababishia taifa hasara ya billioni 63.448

Siku ya jana alipokuwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri za wilaya ya Mbeya na Halmashauri ya Jiji la Mbeya katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Benjamin Mkapa waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amemuagiza Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Mbeya, Emanuel Kiabo kumkamata na kumuhoji aliyekuwa Meya wa Jiji la Mbeya Atanas Kapunga na wenzake 11 kwa tuhuma za kuisababishia Serikali hasara ya sh. bilioni 63.448.
“Serikali hii haiwezi ikawaacha watu hawa ambao wameisababishia hasara kubwa kiasi hiki tena kwa halmashauri moja. Kama wako humu ndani naagiza wakamatwe na waanze kuhojiwa na ambao wamestaafu au kuhamishwa kituo cha kazi wasakwe popote walipo ili nao waje kuhojiwa,” aliagiza waziri mkuu.
 

Share:

0 comments:

Post a Comment

Breaking News

Contact Us

Name

Email *

Message *

Translate

Total Pageviews