Friday, May 12, 2017

Singida United yaendelea kufanya balaa kwenye usajili wachezaji wa nje ligi kuu Tanzania bara.

Timu ya Singida United imeendelea kufanya balaa kwenye usajili wa wachezaji wa kimataifa baada ya kukamilisha usajili wa beki wa timu ya Tusker FC ya Kenya na timu ya taifa ya Uganda ‘The Cranes’ anayefahamika kwa jina Shafik Batambuze. Mchezaji huyo ni wa nne wa kigeni kusajiliwa na Singida United ambayo msimu ujao itacheza ligi kuu Tanzania bara ikiwa chini ya kocha wa zamani wa Yanga Hans van der Pluijm,Tafadwaza Kutinyu, Elisha Muroiwa na Wisdom Mtasa.


 “Tumefikia makubaliano ya kumsajili mchezaji Shafiq Batambuze kutoka Tusker ya Kenya, tumekubaliana kufanya nae kazi kwa miaka miwili akiwa hapa Singida United,” amethibitisha Festo Richard Sanga Chief coordinator wa Singida United ambaye pia ni mmoja wa Wakurugenzi wa timu hiyo.

 “Tunafanya usajili wa nje kwa sababu usajili wa ndani dirisha bado halijafunguliwa, wachezaji wengi wa ndani ambao tunataka kuwasajili wako kwenye makaratasi tayari lakini hadi dirisha litakapofunguliwa ndipo hapo tutawatangaza nani na nani watatua Singida United.......... Tumejipanga kusajili wachezaji saba wa kutoka nje, hadi sasa tumeshasajili wachezaji wanne bado tuna fursa ya kusajili wachezaji watatu lakini kati ya wachezaji watatu, tayari wachezaji wawili tumeshafikia makubaliano kilichobaki ni sisi kumalizia kitu fulani halafu tuwatangaze.” “Kikosi kilichoipandisha timu kipo na kitaendelea kuwepo, tunahitaji kuongeza wachezaji saba wa nguvu wazawa ambao watakuwa wanachukua nafasi ya wachezaji wa kigeni watakapokuwa wanakwenda kwenye nchi zao za taifa kwa sababu wachezaji wote wa kigeni tuliowasajili wanacheza timu za taifa na baadhi yao walicheza michuano ya AFCON 2017.” aliongezea Festo Richard Sanga.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Breaking News

Contact Us

Name

Email *

Message *

Translate

Total Pageviews