Mpaka sasa watu 9 wameripotiwa kufariki baada ya boti iliyokuwa na watalii inayoitwa El Almirante kuzama siku ya jana jijini Medelin nchini Colombia inayokadiriwa kubeba watalii zaidi ya 170.
Mkuu wa kikosi cha uokoaji anayeitwa Margarita Moncada amesema kuwa mpaka sasa watu 9 wameripotiwa kufariki huku wakifanikiwa kuokoa watu 99 na watu wengine 28 hawajulikani walipo mpaka sasa hivi japokuwa juhudi za kuwatafuta zianendelea.
Kwa mujibu wa baadhi ya watalii waliokolewa na baadhi ya wananchi waliofanya mazungumzo na vyombo mbalimbali vya habari wameeleza kuwa sababu ya kuzama kwa boti hiyo ni yenyewe kubeba mzigo mkubwa zaidi ya uwezo wake japokuwa mpaka sasa bado haijatolewa taarifa sahihi ya kuzama kwa boti hiyo.
Waokoaji wakiwa katika harakati za uokoaji. |
0 comments:
Post a Comment