Polisi mjini London wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo gari moja aina ya Van lenye rangi nyeupe limewafuata na kuwagonga kwa makusudi watu 11 ambao walikuwa wakitoka msikitini katika swala la usiku kwenye msikiti wa Finsbury Park ambapo mtu mmoja ameripotiwa kufariki dunia 8 wamepelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu na 2 wameweza kutibiwa eneo la tukio.
Baadhi ya majeruhi wakitolewa eneo la tukio |
Kwa mujibu wa mashahidi walioshuhudia tukio hilo wanasema kuwa gari hilo lilikata kona kwa makusudi kabisa na kuwafata watu hao hatimaye kuwagonga na baada ya hapo watu wawili waliokuwa ndani ya gari hilo walitoka na kukimbia lakini mtu mmoja tu ndiye aliyebaki eneo la tukio mpak polisi walipowasili eneo hilo.
Polisi wamethibitisha kumkamata mwanaume mmoja mwenye miaka 48 ambaye bado hajajulikana jina lake pia wanaendelea na upelelezi wa kuwatafuta watu wawili waliokimbia.
0 comments:
Post a Comment