Friday, May 12, 2017

Unachotakiwa kufahamu kuhusiana Real Madrid pamoja na Juventus kabla ya fainali ya EUFA.

Sasa ni wazi kua washindani wa fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya wameshajulikana ambao ni Real Madrid ya Hispania na Juventus ya Itally hii ni baada ya kushinda michezo yao ya nusu fainali ya michuano hiyo Juventus ndio ilikua ya kwanza kufuzu baada ya kuifunga As Monaco ya Ufaransa kwa jumla ya magoli 4-1 katika michezo yote miwili wakati Real Madrid wakiwatoa majirani zao Atletico Madrid kutoka Hispania kwa jumla ya magoli 4-2 pia katika katika michezo yote miwili Hii imekua fainali yao ya pili katika michuano hii baada ya ile ya maya 20 mwaka 1998 iliyochezwa pale katika dimba la Amsterdam Arena linnaoingiza mashabiki 48500 nchini Uholanzi chini ya mwamuzi Hellmut Krug kutoka Ujerumani juve wakiwa wanaingia katika michuano hiyo mara 3 mafululizo wakati Madrid wakiingia kwa mara ya kwanza tangu kombe hilo lijulikane kama Uefa Champions Leaguue mwaka 1990 ambapo katiaka fainali hii Juventus ilifungwa bao 1 kwa 0 goli la Predrag Mijatovick wakiwa wanashinda kombe lao la 7 la michuano ya Ulaya juve ilikwa chini ya Marcelo lippi wakatin Real wakiwa chini ya Mjerumani Jupp Heyncker.

  Zifuatazo ni tathmini na rekodi za kuangaliwa siku ya fainali hii;

 1.Kocha wa klabu ya Real Madrid Zinedine Zidane alikua katika kikosi cha Juventus kilichofungwa na Madrid sasa anakwenda katika fainali hii akiwa mwalimu wa Madrid 2.Juventus ndio klabu pekee iliyowahi kuingia fainali hii mara 3 mfululizo na kushinda mara moja mwaka 1995-1996,1996-1997,1997-1998 wakishinda mara 1 tu sawa na Ac millan pia ya Italia mwaka 1995-1996,,1996-1997,,1997-1998 3.Kipa wa Juventus Gianluc Buffon ameshatwaa makombe yote katika maisha yake isipokua kombe hilo 4.Sammi Khedira ndiye mchezaji pekee aiyechukua kombe hili na vilabu 2 tofauti Buyern Munich na Real Madrid anatafuta rekodi yake na timu ya 3 trofauti 5.Deffence ya Juve imecheza dk 690 bila kuruhusu kufungwa goli hii nin kabla ya goli la bwana mdogo wa Monaco Kylian Mbappe  6.Baada ya ubingwa mwaka jana Zidane anatafuta ubingwa huo mara ya pili mfululizo  7.Real Madrid wameingia fainali hii mara 15 wakati Juventus wameingia mara 9 8.Christiano Ronaldo amefungwa fainali 1 tu ya mashindano ya ulaya hii ilikua 2008 timu yake ya taifa ya Ureno ilipofungwa na Ugiriki katika michuano ya EURO au michuano ya mataifa ya ulaya 9.Mchezaji Daniel Alves ndio mchezaji pekee aliyecheza fainali nyingi za ulaya kuliko mchezaji yoyote akiwa amecheza fainali 14 uefa champions league 3,uefa europa league 2,,uefa supper cup 5 na ile ya world cup ya klabu mara 3. (By. Buddah Mtanzania)
Share:

0 comments:

Post a Comment

Breaking News

Contact Us

Name

Email *

Message *

Translate

Total Pageviews