Thursday, May 11, 2017

Shabiki aliyeamua kujibadilisha na kukata sehemu za mwili wake ili afanane na viumbe katika filamu..

Luis pardon mwenye miaka 25 anyeishi Buenos Ares nchini Argentina amekuwa shabiki mkubwa wa filamu ya "World of Elves" kwa muda mrefu jambo lililo mpelekea kutumia Euro 25,000 kwa ajili ya upasuaji na kubadiisha mwili wake ili afanane na character wa filamu hiyo.

Luis amebadilisha Nywele zake pia ameweka masikio ya bandia pamoja na kubadilisha rangi ya macho yake ilimradi kufanana na "Elf", Mpaka sasa Luis hutumia Euro 4,000 kila mwezi kwa ajili ya marekebisho ili aendelee kufanana na character huyo "Nina staili yangu ya urembo na ninahitaji kuitimiza kwa ghalama yeyote ile, Nitakata masikio yangu na kuwekewa ya bandia pia nitabadilisha rangi ya macho yangu kufanana na Elf " Alisema Luis kabla ya kujibadilisha kufanana na character huyo wa filamu ya World of Elves.
Wanasayansi wameshauri kuwa kitendo hicho huweza kusababisha magojwa ya kansa kutokana mtu kuwekewa viungo vya bandia katika mwili wake baada ya viungo vyake halisi kukatwa..

Share:

0 comments:

Post a Comment

Breaking News

Contact Us

Name

Email *

Message *

Translate

Total Pageviews