Mechi ya mpira wa miguu iliyopangwa kufanyika jana kati ya Bolucia Dortmund na Monacco ikiwa ni mwendelezo wa mechi za ligi ya mabingwa wa ulaya UEFA imeahirishwa kutokana na mlipuko uliotokea na kuharibu basi la timu ya Dortmund huku ukiacha umemjeruhi beki wa timu hiyo Marc Bartla.
Mlipuko huo umetokea wakati basi hilo lilipokuwa likijiandaa kutoka katika hoteli iliyokuwepo klabu ya Bolucia Dortmund. Police wa eneo hilo wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na wamedai kuwa siku hiyo ilitokea milipuko mitatu lakini bado wako katika uchunguzi ili kujua nini chanzo cha mlipuko huo.
0 comments:
Post a Comment