Askofu mkuu wa kanisa la ufufuo na uzima Josephat Gwajima pamaja na msaidizi wake George Mzava watapandishwa tena kizimbabni leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujitetea katika kesi ya kushindwa kuhifadhi silaha inayowakabili huku wakitetewa na wakili wao Peter Kibatala na Faraja Mangala.
Kesi hiyo ilibidi isikilizwe jana lakini Hakimu Mfawidhi Cyprian Mkela anayesikiliza kesi hiyo hakuwepo hivyo kuahilishwa hadi leo. Katika kesi hiyo askofu Gwajima anakabiliwa na na shitaka la kushindwa kuhifasdhi silaha na risasi anayomiliki kihalali kwa sabab za kiusalama.
0 comments:
Post a Comment