Thursday, July 13, 2017

Tahadhari unayopewa na jeshi la polisi kama mtumiaji wa simu ya mkononi ili kujiepusha kuhusishwa katika matukio mbalimbali ya kihalifu.

Mambo ya kuzingatia kwa mmiliki wa simu ili kujiepusha na hatari pamoja na kuhusishwa katika matukio ya kihalifu.

Usinunue simu za Android kwa mtu usiyemjua Hiyo ni hatari kwani hujui huyo jamaa kaitoa wapi mwisho wa siku unapewa kesi ya wizi au mauaji. Inawezekana simu hiyo iliibiwa kwa mtu aliyeuawa hivyo kitendo cha wewe kuweka line yako katika simu hiyo unaweza kuhusishwa katika tukio hilo.

Usimpe mtu usiye mjua simu yako ya mkononi, Inawezekana mtu huyo akatumia simu hiyo kutekeleza matukio ya kihalifu jambo linaloweza kupelekea wewe kushikiliwa na polisi ama kuhusishwa na matukio hayo moja kwa moja.

Usiokote line ya simu, Watu wengi pindi wanapokutana na laini ya simu iliyotupwa huwa wana tamaduni ya kuokota line hiyo ili kuangalia kiwango cha salio kilichopo. jambo hili linaweza kukuweka katika hatari na kusababisha wewe kuhusishwa na matukio ya kihalifu Simu inapoibiwa mwenye simu kuuawa, line hutupwa, unapoiweka simuni mwako, simuyako inahusishwa na tukio hilo moja kwa moja.

hakikikisha unachana karatasi ya vocha baada ya kuweka salio, Unapoitupa njiani watu wanaweza kufanya tukio la kihalifu ama mauaji, wakachukua karatasi ya vocha ile na kuweka sehemu ya tukio au pale ulipoitupa kukatokea tukio na wewe kuhusishwa na tukio hilo.

Usikubali kumsajilia mtu line ya simu kutumia kitambulisho chako, kumbuka unaposajili line jina lako linahifadhiwa moja kwa moja hivyo kama likitokea tukio lolote la kihalifu na kuhusishwa na moja kati ya laini ulizosajili kwa kitambulisho chako chochote wewe pia utakuwa mtuhumiwa katika kesi hiyo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Breaking News

Contact Us

Name

Email *

Message *

Translate

Total Pageviews