Saturday, June 17, 2017

Utafiti: wanyama wanauwezo mkubwa wakutabiri matetemeko kabla hayajatokea.

Mwanasayansi mjerumani Dr. Wikelski ambaye pia ni mkuu wa chuo cha sayansi cha MayPlank kilichoko nchini ujerumani amebainisha kwa utafiti wake kuwa wanyama wana uweza wa kutabiri tetemeko. 
Dr. Wikelski akiendelea na utafiti 

Mwanasayansi huyo ametoa majibu ya utafiti huo alioufanyia nchini Italy kuanzia mwaka jana katika shamba mojawapo lililopo eneo la Marches nchini humo kwa kutumia baadhi ya wanyama wakiwemo kondoo na mbuzi ambapo amebainisha kubadilika kwa tabia ya wanyama endapo tetemeko la ardhi linapokaribia.


Mwanasayansi huyo amesema kuwa wanyama  huamka usiku na kuanza kutembea huku wakiwa na uwoga pia hata wakati wa mchana wanyama hutembea wakiwa wameachana achana jambo lisilo la kawaida. Nchi ya Italy ni miongoni mwa nchi zinazokumbwa na matetemeko ya ardhi toka mwezi wa nane mwaka jana mpaka mwezi wa kwanza mwaka huu huku yakiacha hasara ya zaidi ya Euro billioni 23 na vifo kadhaa.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Breaking News

Contact Us

Name

Email *

Message *

Translate

Total Pageviews