Kitunguu swaumu ni miongoni mwa viungo
vinavyotegemewa katika kuongenza ladha nzuri kwenye vyakula mbalimbali, lakini wakati kiungo hicho kikitegemewa
katika kuonogesha vyakula wataalam wa tiba asili wanasema ni kiungo hicho ni
dawa endapo kikitumika vizuri.
Miongoni mwa magonjwa ambayo yanaweza kutibika kwa
kutumia kitunguu swaumu ni pamoja na ugonjwa wa kifua, au mkamba, ambapo wataalam wa tiba asili wanasema kuwa, ugonjwa huo
hujitokeza baada ya mifereji inayoingiza hewa mapafuni kupata maambukizi na
kusababisha mgonjwa kukohoa kikohozi mara kwa mara, huku
kikiambatana na makohozi mazito. Ugonjwa mwingine ambao unaweza kutibiwa na kiungo hicho ni kuharisha, hali kadhalika pia husadia kutibumishipa iliyovimba ambayo hujikunja na hivyo kusababisha maumivu makali sana na mara nyingine mishipa hiyo huonekata katika miguu ya watu wa makamo na akina mama wajawazito.Kitunguu swaumu pia hutibu aina mbalimbali za tambaza kama ya mifu, misuli na viungo pamoja na wale watu wenye matatizo ya kupata choo kwa muda wa siku mbili au zaidi anaweza kutibiwa kwa kutumia kitunguu swaumu.
Matumizi na maandalizi ya kitunguu swaumu katika tiba yanategemea aina ya maradhi unayotaka kuyatibu,hivyo basi ni muhimu kuwasiliana na wataalamu wa tiba mbadala ili uweze kupata maelekezo sahihi ya namna ya kuandaa kulingana na ugonjwa unaokusumbua.Kumbuka kama tulivyosema awali kuwa kitunguu swaumu kikipikwa kinapoteza nguvu ya tiba kutegemeana na tiba unayokusudia.
Kumbuka pia kwamba kitunguu swaumu huweza kuchanganywa na vitu vingine mfano;maziwa,asali,habatsouda,juisi,shayiri n.k.kutegemea na maradhi unayotaka kuyatibu na kwa ushauri/maelekezo ya daktari.
0 comments:
Post a Comment