Utafiti mpya uliyofanywa na Chuo Kikuu cha New York, Marekani umegundua
mnyama mwingine ambaye ana ubongo mkubwa sawa na binadamu ambapo utafiti
huo ulionesha jinsi gani mazingira wanayoishi binadamu na Nyani
yanavyoshabihiana na kuwafanya kuwa wanyama pekee wenye ubongo ulio sawa
kwa ukubwa.
Mkuu wa utafiti huo Alex Decasian alizungumza na BBC >>> “Nyani
hasa jamii ya Orangutans wana ubongo ulio sawa na binadamu kwa kuwa
hupitia changamoto zinazofanana, nyani mwenye umri mkubwa ana ubongo
mkubwa zaidi kuliko Nyani mtoto, hii inasadia katika ulinzi wa jamii yao
na kutatua matatizo kama ugomvi”
Utafiti huo pia ulionesha nyani anayekula matunda ana ubongo mkubwa
zaidi ukilinganisha na nyani anayekula majani na mizizi ambapo
Mwanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Oxford amesema ubongo mkubwa
humtofautisha nyani na wanyama wengine katika uelewa wa mambo, kuwa na
huruma na kutambua majukumu yao.
0 comments:
Post a Comment