Wanajeshi wawili walio katika mahusiano ya kimapenzi Marinna Rollins na Jarren Heng wakazi wa North Carolina nchini Marekani wamefunguliwa mashtaka baada ya kumning'iniza mbwa wao na kumpiga risasi mara tano kwa kukusudia na baadae kumzika. Tukio la kumpiga risasi mbwa huyo limefanywa na Rollins na hiyo ni baada ya kuzungumza na boyfriend wake Jarren kupitia mtando wa facebook na yeye kulidhia jambo hilo kufanyika.
Polisi wanaeleza kuwa kabla ya tukio hilo walipiga picha ndani ya mavazi yao ya kijeshi akiwa na mbwa huyo kama ishara ya kumuaga mbwa huyo kisha Jarren aliondoka na baadae ndipo Rollins alipotekeleza tukio hilo.
Rollin alistaafu jeshi mwezi wa kwanza mwaka huu kwa sababu za kiafya na imeripotiwa kuwa alishawahi kupata mtatizo ya kisaikolojia ikiwa miongoni mwa sababu zilizopelekea yeye kuwahi kustaafu.( source. Sky News)
0 comments:
Post a Comment