Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA na Kiongozi wa kambi
rasmi ya upinzani Freeman Mbowe amtuhumu
Rais John Magufuli pamoja na waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuhusika na
alichodai kuwa ni kukiukwa kwa taratibu za uchaguzi wa kuwapata wawakilishi katika bnge la afrika mashariki
Mbowe ameongea hayo jana usiku mara baada ya kutoka kwenye ukumbi wa
bunge ambapo amedai kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Rais Magufuli
kuhusika kwenye mchakato wa kuyakataa majin ya wagombea wa Chadema.
Mbowe amesema kuwa, wao hawatakubaliana na hilo kwa sababu Spika wa
Bunge amekiuka kanuni za bunge, na uchaguzi wote ulikuwa wa kasoro.
Wagombea waliopendekezwa na Chadema Wenje Na Masha ambao walipigiwa kura za
hapana katika kuwania kuiwakilisha Tanzania katika bunge la Afrika
Mashariki. Nje ya ukumbi wa Bunge Kiongozi wa kambi
rasmi ya upinzani Bungeni Freeman Mbowe ameongea na waandishi wa habari
na kusema kuwa hawakubaliani na matokeo na watakwenda Mahakamani kudai haki yao.
Wednesday, April 5, 2017
Home »
» Mbowe awatuhumu JPM na Majaliwa kwa kuhusika kutochaguliwa wabunge wa upinzani bunge la Afrika Mashariki.
0 comments:
Post a Comment