Raisi wa marekani Donald Trump amemshambulia kwa maneno na kumkosoa meya wa jiji la London Sadiq Khan baada ya shambulio la ugaidi kutokea. kupitia akaunti yake ya twitter Trump aliandika maneno yanayoonyesha kumkosoa meya huyo mara baada ya interview aliyoifanya meya wa jiji hilo katika kituo kimoja cha televisheni na kuwaasa watu kutohofia hali ya polisi kuwa wengi kwa sasa katika jiji hilo na kwamba jiji la London ndio jiji lenye usalama zaidi duniani kwa sasa. Trump aliandika kuwa alichokisema meya huyo ni kisingizio kisicho na msingi japokuwa vyombo vya habari vinaangaika na kujitahidi kukipromote, maneno ambayo yalijibiwa na meya wa jiji hilo kwa kusema kuwa kwa sasa yeye ameelekeza umakini wake katika kulifanya jiji hilo kuwa bora na salama zaidi.
Viongozi wengi wameonyesha kutofurahishwa na maneno hayo ya raisi huyo na kusema kuwa haikuwa sawa kwa Trump kuandika maneno kama yale kwa meya wa jiji hilo katika kipindi hiki ambacho watu wote wanajaribu kuweka hali ya amani katika usawa.
0 comments:
Post a Comment