Monday, June 5, 2017

Polisi uingereza wataja majina ya watu wawili waliohusika na shambulio la kigaidi katika daraja la London.

Polisi nchini uingereza wamewataja Khuram Shazad Butt na Rachid Redouane kuwa ndio waliohusika na shambulio la kigaidi katika daraja London. Hatua hii inaonyesha kuwa tayari polisi wamefikia hatua ambayo wataweza kutoa maelezo yaliyo kamili kuhusiana na tukio hilo. Khuram Shazad Butt miaka 27 ni raia wa Pakistani aliyeingia nchini uingereza akiwa na umri mdogo ambapo mpaka sasa anatambulika kwa jina la Abu Zaitun ama Abu. Rachid Redouane yeye ana miaka 30  amezaliwa mwaka 1986 akiwa ni mchanganyiko wa nchi mbili  Morocco pamoja na Italy. Polisi wamesema kuwa Rachid alikuwa akitumia jina la Rachid Elkhdar huku akitumia vyeti feki vya kuzaliwa vilivyoonyesha kuwa ana umri pungufu kwa miaka mitano (5).
Mpaka sasa bado polisi wako katika uchunguzi ili kumbaini mtu wa tatu anayesemekana kuhusika katika shambulio hilo la kigaidi.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Breaking News

Contact Us

Name

Email *

Message *

Translate

Total Pageviews