Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limejiweka kando kuhusu
sakata la majina 65 ya watu waliyotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda, akiwatuhumu kujihusisha na dawa za kulevya.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini jana, Kamanda wa
Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro, alipoulizwa kuhusu
mwitikio wa wahusika kwenda polisi kama walivyotakiwa na Makonda,
alisema suala hilo sasa haliko chini yake.
Alisema tayari walishakabidhi majina ya watuhumiwa kwenye ofisi ya
Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya baada ya Rais John Magufuli kumteua
Kamishna Mkuu, Rogers Sianga kuiongoza.
Kamishna Sirro alisema wanawashikiliwa watuhumiwa 105 wa dawa za kulevya
ikiwamo bangi na pombe ya gongo. Alisema katika msako wao wamekamata
dawa za kulevya kete 413 (bila kutaja ni aina gani), puli 50, misokoto
ya bangi 86 na gongo lita 45.
Awamu ya tatu ya vita ya Makonda dhidi ya dawa za kulevya inahusisha
majina 97 ya watu ambao hayakutajwa hadharani na Mkuu huyo wa Mkoa
badala yake aliyakabidhi kwa Kamishna Sianga Februari 13 kwa ajili ya
uchunguzi zaidi.
Source. Muungwana.blogspot
Wednesday, March 1, 2017
Home »
» Polisi wajiweka kando sakata la majina 65 ya makonda.
0 comments:
Post a Comment