Tuesday, March 14, 2017

Wafanyakazi 9 wasimamishwa TBC kwa kurusha habari ya ungo.



Hatua hiyo imechukuliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TBC, Ayubu Rioba kutokana na habari iliyosomwa na mtangazaji wa TBC Gabriel Zacharia iliyokuwa ikiongelea hatua ya raisi wa Marekani Donald Trump kumsifia raisi wa tanzania DR. John Pombe Magufuli kutokama na uchapakazi wake na hatimaye kutoa ruhsa kwa watanzania kuingia nchini Marekani.

Habari hiyo ilitangazwa na TBC kwenye taarifa yao ya usiku mwishoni mwa wiki iliyopita. Mpaka sasa watangazaji 9 wamesimamishwa kazi kutokana na kushiriki kuandika na kuitangaza habari hiyo ya uongo.
Waliosimamishwa kazi ni pamoja na mtangazaji aliyeisoma habari hiyo, Gabriel Zakaria na wengine ni Elizabeth Mramba, Prudence Constantine, Dorothy Mmari, Ramadhan Mpenda, Leya Mushi, Alpha Wawa, Chunga Ruza na Judica Losai.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Breaking News

Contact Us

Name

Email *

Message *

Translate

Total Pageviews